Effective Strategies for Academic Leadership in Primary Education

tet 06101 n.w
1 / 25
Embed
Share

Explore the importance of effective leadership in primary education, including strategies for discipline management and academic enhancement. Understand the concept of leadership in education and the role of school leaders in fostering a conducive learning environment. Learn about engaging stakeholders and promoting pedagogical practices for academic success.

  • Academic leadership
  • Primary education
  • Discipline management
  • Stakeholder engagement
  • Pedagogical practices

Uploaded on | 0 Views


Download Presentation

Please find below an Image/Link to download the presentation.

The content on the website is provided AS IS for your information and personal use only. It may not be sold, licensed, or shared on other websites without obtaining consent from the author. If you encounter any issues during the download, it is possible that the publisher has removed the file from their server.

You are allowed to download the files provided on this website for personal or commercial use, subject to the condition that they are used lawfully. All files are the property of their respective owners.

The content on the website is provided AS IS for your information and personal use only. It may not be sold, licensed, or shared on other websites without obtaining consent from the author.

E N D

Presentation Transcript


  1. TET 06101 UONGOZI KATIKA ELIMU Hapa Kazi Tu Mwl. Msuri, I. S

  2. 1.2.2 KUBAINI MIKAKATI YA KUDHIBITI NA KUIMARISHA TAALUMA KATIKA ELIMU YA MSINGI MATOKEO WEZESHI (a) Kubaini mikakati ya kudhibiti nidhamu na kuimarisha taaluma katika elimu ya msingi. (b) Kufafanua umuhimu wa mikakati ya kudhibitinidhamu shuleni.

  3. ( c ) Kuainisha mikakati ya kudhibiti nidhamu shuleni. (d) Kubainisha wadau watakaoshirikishwa katika kutekeleza mikakati husika ili kudhibiti nidhamu na kuimarisha taaluma shuleni.

  4. Dhana Ya Uongozi Dhana ya uongozi huelezwa tofauti na wataalamu mbalimbali wa masuala ya elimu. Wataalamu wengi wanaeleza kuwa uongozi ni hali ya ushawishi katika matumizi ya nafasi aliyonayo mtu kuwashawishi wengine katika kutekeleza malengo waliyojiwekea.

  5. Wills & Rollie (2007) uongozi ni matumizi ya nafasi inayohusisha mambo ya uhamasishaji, kushirikisha, kuratibu, kutia moyo, kumotisha na kuwapongeza wale wanaofanya vizuri katika kutekeleza malengo waliyojiwekea. Hivyo kazi kubwa ya kiongozi ni kuonyesha njia ili kufikia malengo.

  6. Uongozi Katika Elimu Uongozi ni sanaa, talenti, kaliba au sayansi inayotumika kutengeneza mazingira wezeshi(supportive learning environment) ya kujifunzia na kufundishia (Day & Harris, 2007). Hurber (2004) uongozi katika elimu ni zoezi la au mchakato wa kuwahamasisha watu au kikundi cha watu katika kutekeleza malengo ya pamoja waliyojiwekea shuleni.

  7. Uongozi katika shule zetu unapaswa kujengwa katika misingi ya majidiliano kati ya M/Mkuu, walimu, wanafunzi pamoja na shule kwa ujumla kama taasisi. Walimu wakuu wanayo nafasi kubwa katika kuhakikisha kuwa shule inafanya vizuri kitaaluma (to develop sound pedagogical practices in a school).

  8. Sergiovanni (1998) viongozi katika elimu wana kazi: i. kuwaendeleza kitaaluma ii. Kuwaendeleza kitaalam iii. Kuwaendeleza kijamii hayo yote ni katika kuimarisha maarifa na ujuzi wa mwalimu na wanafunzi katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji i.e kusaidia kuboersha kazi zao za darasani.

  9. Kazi kubwa ya uongozi wa shule ni kusimamia shughuli zote za kila siku katika uendeshaji wa shule. Mfano kuhamasisha, kushirikisha, kupanga , kuongoza ufundishaji na kazi zote katika shule.

  10. Ni muhimu kwa uongozi wa shule kumfanya kila mtu/mdau ashiriki kikamilifu katika kusimamia taratibu za elimu. Mf. Kuhamasisha rasilimali hususani pesa katika kuhakikisha vifaa vya kufundishia na kujifunzia zinapatikana.

  11. Hivyo malengo ya kozi ni: i. Kupata maarifa na uelewa mpana juu ya uongozi katika shule za msing. ii. Kubaini na kuelewa kazi tofauti za kiongozi katika shule za msingi ili kuhakikisha uendeshaji wa shule ni mzuri na kunatolewa elimu bora. iii. Kuwa viongozi mahiri wa elimu (pedagogical leadership). iv. Kuwa na mikakati ya kiongozi, maarifa na ujuzi katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji shuleni.

  12. (a) Kubaini mikakati ya kudhibiti nidhamu na kuimarisha taaluma katika elimu ya msingi. Lengo la kipengele hiki ni kutoa uelewa juu ya tabia mbalimbali walizonazo wanafunzi na jinsi ya kuizuia ili kuboresha elimu. Mara nyingi unaweza kusikia kauli tofauti za walimu juu ya mienendo ya wanafunzi wao wakiwa shuleni na hata katika jamii inayowazunguka

  13. Hivyo nidhamu ni kitu muhimu sana kwa wanafunzi kwa walimu wao kwa sababu hupelekea wanafunzi wakafanya vizuri katika masomo yao au kitaaluma (MOC, 2000). Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa nidhamu ni hali au jinsi mtu anavyoweza kuonekana, kutenda au anavyojichukulia akiwa peke yake au mbele ya watu (behaves or acts) (MOC, 2000).

  14. Uongozi katika elimu ni muhimu kubainisha mikakati ambayo itadhibiti nidhamu na kuboresha taaluma. Mikakati hiyo lazima ijenge mazingira ambayo yatawahamasisha wanafunzi kusoma kwa juhudi pamoja na walimu kufundisha kwa bidii madarasani (to enhance pupils learning and development and teacher learning and classroom effectiveness).

  15. Mikakati hiyo ya kudhibiti nidhamu na kuimarisha taaluma ni lazima ionyeshe njia na mwelekeo wa ushiriki wa wadau wote muhimu katika kusimamia elimu mashuleni. Hivyo, Uongozi wa shule ni muhimu ukatengeneza mikakati, taratibu na kanuni anuai katika kuhakikisha kuwa shule inaendeshwa kulingana na sera, kanuni na maelekezo ya Wizara ya Elimu.

  16. Mikakati Ya Kudhibiti Nidhamu Na Kuimarisha Taaluma Katika Elimu Ya Msingi. 1. Kuimarisha kamati ya nidhamu shuleni. Kamati hii isimamiwe na walimu waadilifu ambao watakuwa mfano wakuigwa shuleni na jamii kwa ujumla.

  17. 2. Kuimarisha Kamati Ya Taaluma. Taaluma ndio msingi mkuu (core?primary functions of the school) wa kuwepo walimu na wanafunzi shuleni. Kamati iwahusishe walimu wenye uwezo mzuri kitaaluma na wasio na chembe ya shaka katika ufundishaji wao na kazi zote za ndani na nje ya darasa.

  18. 3. Kuimarisha Ushirikiano Katika Ya Walimu Na Wazazi. -M/mkuu na walimu wenzake yawapasa kuifanya shule kuwa ni kituo cha malezi na kuwaelimisha wazazi kuwa shule ni sehemu ya kijiji/jamii na sio kisiwa (Wizara ya Elimu ya Taifa (WET), 1995). - Bray (2003) anaseme ushirikiano mzuri hutegemea msingi wa wazazi kushiriki kikamilifu katika kazi za shule na hupelekea uwajibikaji wa pamoja.

  19. - Kuwakaribisha wazazi kutoa mawaidha , malezi na utamaduni wa jamii. - Uongozi uwashirikishe wazazi mapema unapogundua makosa ya awali ya mwanafunzi ili chanzo chake kieleweke mapema na kupata utatuzi mapema kwa pamoja.

  20. Tafiti zinaonyesha kuwa ushirikiano mzuri katika ya walimu, wazazi na jamii kwa ujumla hupeleke watoto kujifunza kwa furaha na hupata matokeo mazuri katika mitihani yao (Booth & Dunne, 1996)

  21. 4.Kudumisha Mawasiliano - Ni muhimu kuimarisha mawasiliano kati ya shule na wazazi katika kudumisha nidhamu na taaluma shuleni. - Mawasiliano yakiimarishwa huleta maana muafaka ya ushawishi kwa mtu binafsi au kikundi cha watu katika mambo ya shule (Hoy & Miskel, 2001).

  22. Umuhimu wa mawasiliano. - huwezesha kutoa malengo ya shule - hufanikisha majukumu yanayohusu uratibu wa shughuli za shule - Husaidia kusambaza habari kwa wahusika wote kuhusu shule. - husaidia katika kufanya maamuzi - Humotisha na hushawishi wadau wa elimu kuhusu shule , malengo na majukumu ya shule yao.

  23. 5. Vikao vya Wazazi - Vikao ni nguzo muhimu sana katika uendeshaji wa shule. - Uongozi wa shule unapaswa kujua umuhimu wa familia katika kusimamia nidhamu na taaluma shuleni (WET, 1995). - Lengo kuu la vikao ni kutoa fursa ya kubadilishana mawazo, kufafanua baadhi ya mambo na kuainisha mikakati mbalimbali ya kuboresha mazingira ya shule.

  24. 6. Siku Ya Wazazi (Parents Day) - huweza kufanyika kila muhula au mara2 kwa mwaka ili: i. Wazazi wapate nafasi ya kuizuru shule, kuona kazi za watoto wao madarasani na nje ya darasa na kupata fursa ya kutoa maoni yao panapohitajika. ii. Walimu watoe taarifa zao kwa wazazi kuona mbinu zipi zingetumika kudumisha nidhamu na kuinua maendeleo ya shule kwa ujumla.

  25. 7.Dira, Malengo Na Madhumni Ya Shule Yawe Wazi (Shared Vision)

More Related Content