Leadership in Educational Change Management: Guiding School Transformations

tet 06101 n.w
1 / 27
Embed
Share

Explore the concept of change management in education leadership, focusing on overseeing changes in schools. Understand the importance of leading change as an educational leader and analyze the associated challenges. Learn how leaders play a crucial role in shaping school culture and managing transformations effectively.

  • Education
  • Leadership
  • Change Management
  • School Transformation
  • Challenges

Uploaded on | 0 Views


Download Presentation

Please find below an Image/Link to download the presentation.

The content on the website is provided AS IS for your information and personal use only. It may not be sold, licensed, or shared on other websites without obtaining consent from the author. If you encounter any issues during the download, it is possible that the publisher has removed the file from their server.

You are allowed to download the files provided on this website for personal or commercial use, subject to the condition that they are used lawfully. All files are the property of their respective owners.

The content on the website is provided AS IS for your information and personal use only. It may not be sold, licensed, or shared on other websites without obtaining consent from the author.

E N D

Presentation Transcript


  1. TET 06101 UONGOZI KATIKA ELIMU KUSIMAMIA MABADILIKO KATIKA SHULE Mwl. Msuri, I. S P.MEELA HOMELIBRARY

  2. 3. Kufafanua Dhana Ya Usimamizi Wa Mabadiliko Katika Uongozi. a). Kueleza dhana ya kusimamia mabadiliko (change management) atika shule. b). Kueleza umuhimu wa kusimamia mabadiliko kama kiongozi. c). Kuchambua changamoto zinazoendana na mabadiliko. P.MEELA HOMELIBRARY

  3. a). Kueleza dhana ya kusimamia mabadiliko (change management) atika shule. Dhana ya Mabadiliko - Neno mabadiliko hutumika katika elimu kwa maana ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji shuleni. - Wakati mwingine huelezea namna ya kuboresha mazingira ya shule ili ufundishji na ujifunzaji uweze kufanyika kwa ufanisi . P.MEELA HOMELIBRARY

  4. - Mabadiliko yote hupitia hatua mbalimbali ili yaweze kukubalika katika shule ama taasisi. Mambo ya muhimu yanayolenga kuboresha elimu/masomo ni lazima yawe na dira, maono (vision) na malengo ya mabadiliko. P.MEELA HOMELIBRARY

  5. -Tunapozungumzia mabadiliko maana yake ni kubadilisha utamaduni, mazoea au utendaji wa kazi na mahusiano katika shule. Utamaduni wa shule ni elementi ya muhimu sana katika mabadiliko shuleni (Muijs, harris & Chapman, 2005). -Kila shule ina utamaduni wake ambao huitofautisha shule moja na nyingine. - Ni vizuri kutambua kuwa mabadiliko yote sio maboresho lakini maboresho yote ni mabadiliko. P.MEELA HOMELIBRARY

  6. Dhana ya Kusimamia Mabadiliko - Kimsingi ili mabadiliko yaweze kutokea na kufanikiwa shuleni anahitajika kiongozi mwenye utayari na mwenye maono (Transformational &Visionary Leader). - Kiongozi mwenye maono husoma mazingira ya shule kwa umakini ili kubaini shule inahitaji kitu gani na watu gani watahusika katika kufanikisha mabadiliko yatakayo tokea shuleni. -Viongozi wanayo nafasi kubwa ya kutengeneza utamaduni wa kupokea na kusimamia mabadiliko (Hallinger & Kantamara, 2001). P.MEELA HOMELIBRARY

  7. -Dhana ya kiongozi kusimamia mabadiliko ni muhimu sana kwani mara nyingi viongozi ndio wanaopaswa kuwajibika kwa kila jambo linaloendelea shuleni -Viongozi hutengeneza na kuusimamaia utamaduni wa shule katika kazi za kila siku. -Unapoongelea kusimamia mabadiliko unazungumzia kubadilisha utanaduni, mazoea, utendaji na pengine mahusiano ya wadau wote shuleni. P.MEELA HOMELIBRARY

  8. - Walimu Wakuu pia hupaswa kujua watu/wadau wanaofikiri ni muhimu kushiriki katika mchakato wa mabadiliko, wanaojua mahitaji ya mabadiliko na wenye kuwajibika katika mabadiliko hayo na kujihisi kuwao wao ndio wamiliki wa mabadiliko hayo ili yaweze kuleta maana. - Ili mabadiliko yaweze kufanikiwa vizuri ni muhimu kutengeneza utamaduni wenye mahusiano mazuri unaochochea watu kupokea mabadiliko kwa wepesi. (mutual adaptation) P.MEELA HOMELIBRARY

  9. - Kitu muhimu katika kusimamia mabadiliko ni kubadilisha utamaduni wa kufanya kazi kwa mazoea na hii hupelekea shule kujipambanua kutokana na muundo wa uongozi, wajibu wa kila mtu, mbinu za mawasiliano na kushirikiana katika kila jambo. - Kiongozi anayekubali na kuongoza mabadiliko huitwa mwanamabadiliko au transformational leader ambaye hutengeneza na kuisimamia vizuri dira ya maendeleo na kuwavutia wale anaowaongoza. - Kitu muhimu ni kuyatafsiri kwa vitendo hayo mabadiliko (Spillane, 2000). P.MEELA HOMELIBRARY

  10. Kwa nini mabadiliko 1. Kufikia malengo ya elimu yanahitaji wanafunzi kufanya vizuri kitaaluma. 2. Malengo ya elimu ni makubwa hivyo ni lazima kuwepo matatizo katika mchakato wa kuyafikia. 3. Kuboresha mazingira ya ufundishji na ujifunzaji 4. Mabadiliko ya sayansi na teknolojia mf. TEHAMA. 5. Mabadiliko ya mtaala ambayo huhitaji walimu kubadilika katika utendaji wao. 6. Mahitaji ya jamii 7. Uhaba wa rasilimali katika mchakato wa utekelezaji wa mtaala. P.MEELA HOMELIBRARY

  11. Hatua za mabadiliko - Ipo mitizamo mingi inayoelezea hatua za kupitia katika kufanya mabadiliko. 1. Connolly, Connolly & James (2000) katika andiko lao Leadership in Eduacational Change - Wameonesha kuwa kiongozi huongoza mabadiliko katika hatua tatu: 1. Pre-acceleration stage- mwanzo wa mabadiliko. - Kiongozi hubadilisha utamaduni na kuongoza migongano katika taasisi, kuhamasisha ubunifu na kubadilika. P.MEELA HOMELIBRARY

  12. 2. Acceleration stage-rapid change- (wakati wa mabadiliko) Mabadiliko yanakolea mwendo. - Kuongoza mazingira ya mabadiliko - kubadilisha mfumo, muundo wa uongozi na wajibu - kujenga umoja na ushirikiano - kuhamasisha mijadala ya kitaaluma (professional dialogue). - kuyaingiza mabadiliko katika taasisi na jamii kwa ujumla. P.MEELA HOMELIBRARY

  13. 3. Post acceleration baada ya mabadiliko. - Hii ni hatua muhimu kwa viongozi katika kuyasimamia, kuyaenzi na kuyaboresha mabadiliko pale inapobidi. - Uongozi hujenga utamaduni mpya. - Kuendelea kubadilika katika mfumo wa uongozi wa uwajibikaji P.MEELA HOMELIBRARY

  14. 2. Mtizamo wa pili katika hatua za mabadiliko ni ule wa Anderson na Wenderoth (2007)- kitabu choa cha Facilitating Change: Reflection On Six Years Of Education Development Programming In Challenging Environment - Hawa wameelezea kitu kinachoitwa mzunguko wa mabadiliko (change circle) P.MEELA HOMELIBRARY

  15. - Msisitizo ni kwamba, viongozi wanapotaka kuanzisha mabadiliko ni vizuri kujua mzunguko wa mabadiliko. - Kwa mtizamo wao, kuna hatua nne za kuzingatia katika kufanya mabadiliko shuleni. P.MEELA HOMELIBRARY

  16. Hatua hizo ni: 1. Denial Migongano - kukataa, kugoma, kutokubaliana n.k 2. Resistance Kupambana - kusuguana, kuwa na upinzani, kuwepo makundi, kushindana, kuvutanana n.k P.MEELA HOMELIBRARY

  17. 3. Exploration of change utafiti juu ya mabadiliko - kuangalia kitakachotokea, kuchunguza,, ugunduzi, majaribio n.k 4. Commitment Kuwajibika - Utayari, kufurahia, kuahidi, kuwa na uhakika, utiifu, nidhamu n.k P.MEELA HOMELIBRARY

  18. Jinsi ya kusimamia mabadiliko katika shule 1. Uongozi mzuri ambao utakuwa chanzo cha mabadiliko (Transformational leadership). Uongozi ni ufunguo wa kufanikisha au kuharibika mabadiliko (Fullan, 2001) Viongozi wanatakiwa kuwa tayari kubadilika kulingana na mahitaji ya mazingira. 2. Kutengeneza dira, maono na malengo ya pamoja (developing shared vision & goals) Mabadiliko lazima yaendane na dira pamoja na maono yanayoongoza hayo mabadiliko (best leadership build shared vision (Anderson & Wenderoth, 2007). P.MEELA HOMELIBRARY

  19. 3. Kuwashirikisha wazazi, wanafunzi na jamii kwa ujumla katika hatua za mwanzo za mabadiliko. -Katika kuleta mabadiliko, viongozi wanapaswa kuwashirikisha wadau wote muhimu. -Utamaduni wa kushirikiana na kupanga pamoja hurahisisha usimamiaji wa mabadiliko (Geisjel & Meijers, 2005). P.MEELA HOMELIBRARY

  20. 4. Kuweka mipango ya maendeleo ya shule inayokubali mabadiliko. -Kikubwa katika kupanga ni kujenga mazingira rafiki/wezeshi yanayopokea mabadiliko shuleni. -Ni vizuri viongozi wakawaongoza watu wote kwenye kupanga, kutekeleza na kufanya marekebisho yanapohitajika (Spillane, 2000). P.MEELA HOMELIBRARY

  21. 5. Kuweka Wazi Mfumo, Muundo Na Wajibu Wa Kila Mtu Katika Kusimamia Mabadiliko (Open Organization Structure). - Mifumo ikiwa wazi husaidia kujenga imani na kuaminiana. -Ili kufanikiwa katika kusimamia mabadiliko ni vyeme viongozi wakajenga uaminifu katika taasisi wanazoongoza (Louis, 2006). P.MEELA HOMELIBRARY

  22. 6. Kuwepo Ufuatiliaji, Usimamizi, Upimaji Na Tathmini Ya Mabadiliko Shuleni. -Viongozi wanapaswa kuwa na uwezo wa kuanzisha, kufuatilia na kuongoza mchakato wa mabadiliko (Geisjel & Meijers, 2005). P.MEELA HOMELIBRARY

  23. 7. Mabadiliko Yanayotokea Shuleni Lazima Yasisitize Ufundishaji Na Ujifunzaji Ili Kupata/Kufikia Matarajio Ya Elimu Bora. - Viongozi wanatakiwa kuwa tayari kwa hasara (take risk) itakayotokana na mabadiliko katika kuboresha matokeo ya wanafunzi (Connolly, Connolly & James, 2000). 8. Kusherehekea Mafanikio Pamoja (together celebrate success). P.MEELA HOMELIBRARY

  24. 9. Kujenga Urafiki Na Shule Na Jumuiya Zinazoizungusha Shule (benchmark & networking). 10. Kuwa Na Utaratibu Wa Kujiendeleza Na Kuendelea Kujifunza Kwa Walimu (Continuous professional development). - Viongozi wanapaswa kuifanya shule kuwa ni sehemu ya walimu kujiendeleza na kuboresha utendaji wao (Geisjjel & Meijers, 2005). P.MEELA HOMELIBRARY

  25. 11.Kujenga Mbinu Nzuri Za Mawasiliano Kati Ya Kiongozi Na Wadau Wa Shule. - Kuimarisha mawasiliano na kuendelea kuwafahamishana kila hatua ya mabadiliko/ maendeleo inavyofanyika ni kiungo muhimu katika kipengele cha kuongoza na kusimamia mabadiliko. (Communicating continually about the change is a vital aspect of leading change) (Anderson & Wenderoth, 2007) P.MEELA HOMELIBRARY

  26. 12. Kuyaingiza Mabadiliko Katika Utamaduni Wa Shule (institutionalization of change). - Mabadilko yaingie katika mazingira yote muhimu ya shule (Connolly, Connolly & James 2000). P.MEELA HOMELIBRARY

  27. MWISHO mwajifya HapaKaziTu (Magufuli, 2015). P.MEELA HOMELIBRARY

Related


More Related Content