
Transformation of Gender Roles in Agricultural Practices at Tandai Village, Tanzania
"Discover how the villagers of Tandai in Tanzania have reshaped traditional gender roles in agriculture, promoting gender equality and collaborative decision-making within families. Learn how they are embracing sustainable development goals for gender responsiveness. Witness a progressive shift towards inclusivity and empowerment."
Download Presentation

Please find below an Image/Link to download the presentation.
The content on the website is provided AS IS for your information and personal use only. It may not be sold, licensed, or shared on other websites without obtaining consent from the author. If you encounter any issues during the download, it is possible that the publisher has removed the file from their server.
You are allowed to download the files provided on this website for personal or commercial use, subject to the condition that they are used lawfully. All files are the property of their respective owners.
The content on the website is provided AS IS for your information and personal use only. It may not be sold, licensed, or shared on other websites without obtaining consent from the author.
E N D
Presentation Transcript
KONGAMANO LA JINSIA NA HABARI 2018 WANAKIJIJI WALIVYOBADILI HADITHI YA MAMA KULIMA, BABA KUUZA Gazeti:Majira (Tanzania, Dar es Salaam, 23/8/2018) Mfumo dume siku za nyuma ulitukosesha haki kabisa ya kuwa na maamuzi katika familia, hususani baada ya kuvuna mazao kama iliki, karafuu, pilipili manga na mazao mengine, ambaye alikuwa na maamuzi ni baba, kwani alitumia nafasi hiyo kwenda kuuza na kufanya matumizi bila ushirikishwaji, lakini kutokana na elimu ya mara kwa mara wamebadilika sana, anasema Mariam Ilyasa mkazi wa Kijiji cha Amini Kata ya Kinole. Acceleration of Gender-responsive Sustainable Development Goals localisation
MUHTASARI Mara nyingi katika jamii kadhaa hapa nchini Tanzania kazi za kilimo zimekuwa zikifanywa na akinamama na wanaume kujitokeza wakati wa kuvuna na kuuza mazao. Hata hivyo, hadithi ni tofauti kabisa katika Kijiji cha Tandai Kata ya Kinole, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro mkoani Morogoro, ambapo wanakijiji wamejiwekea mfumo unaozingatia usawa wa kijinsia.Mfumo ambao baba na mama wanashiriki kwa nafasi sawa katika kilimo, uvunaji, uuzaji na upangaji wa matumizi ya fedha kwa ustawi bora wa familia zao. Wanakijiji hao wanajishughulisha na kilimo cha viungo mbalimbali zikiwemo iliki, mdalasini, pilipili mtama, binzari na karafuu. Utafiti wangu niliona umeibua jambo la kipekee sana katika hatua ya kuondoa dhana potofu kuwa, kinamama wao ndiyo wenye jukumu la kulima na kinababa kutumia kipato. Hivyo hii inakuwa moja ya hatua nzuri na mfano wa kuigwa Acceleration of Gender-responsive Sustainable Development Goals localisation
TATHIMINI Alama (1-10) 10 Mada inayoangaziwa katika makala inahusisha usawa wa kijinsia moja kwa moja. Inajumuisha jinsia zote (kinamama na kinababa) 10 10 Makala inajumuisha wadau wote 10 Jinsia zote zinafanya kazi kwa ushirikiano Makala inaondoa dhana potofu kuhusiana na unyanyasaji 10 10 Makala inazijengea jamii na makundi yote uwezo 10 Mambo yote ya kitakwimu yanatokana na maelezo ya walengwa Makala imetoa nafasi sawa kwa jinsia zote Mawazo yote yaliyomo ni kutokana na walengwa na wadau husika Makala inaongeza hamasa kwa jamii TOTAL 10 10 10 100
MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU Usawa wa kijinsia ni miongoni mwa maelekezo yaliyomo kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya Umoja wa Mataifa ambayo yalianza mwaka 2015 na yatafikia ukomo mwaka 2030, ambapo kusudio langu lilikuwa kuona namna wanakijiji wa Kijiji cha Tandai Kata ya Kinole wanatekeleza Lengo namba 5 A. Lengo hilo linaelezea umuhimu wa kufanya mageuzi ya kuwapa wanawake haki sawa na rasilimali za kiuchumi,pamoja na upatikanaji wa umiliki na udhibiti wa ardhi na aina nyingine za mali,huduma za kifedha,urithi na maliasili,kwa kuzingatia sheria za Kitaifa. Nilifanikiwa sana kujumuisha lengo hilo na ushiriki wa wanakijiji hao katika shughuli zao za kilimo. Acceleration of Gender-responsive Sustainable Development Goals localisation
USULI/BACKGROUND Utafiti wangu ulikuwa unaangazia namna ambavyo ushiriki wa wanawake katika kilimo cha viungo mbalimbali ikiwemo mdalasini, iliki, pilipili manga, karafuu na binzari unavyowahusisha wanawake na wanaume kuanzia hatua za awali, mavuno na hata kwenda kuuza katika Kijiji cha Tandai Kata ya Kinole, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini. Ikiwa na lengo la kutambua pia namna wanakijiji hao wanadumisha usawa wa kijinsia katika utekelezaji wa shughuli za kilimo hicho. Hii ni kwa sababu usawa wa kijinsia ni miongoni mwa maelekezo yaliyomo kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya Umoja wa Mataifa ambayo yalianza mwaka 2015 na yatafikia ukomo mwaka 2030. Baada ya uchunguzi nilioufanya nilibaini kuwa, wanakijiji hao wao wameenda mbali zaidi kwani ile dhana ya kuwa wanawake jukumu lao ni kulima na kinababa kwenda kuuza kwao walishafanikiwa kuondoka huko. Makala hiyo ambayo ilichapishwa katika gazeti la kila siku la MAJIRA inakuwa mfano mzuri katika kuimarisha ustawi wa usawa wa kijinsia kutokana na ukweli kwamba mara nyingi katika jamii kadhaa hapa nchini Tanzania kazi za kilimo zimekuwa zikifanywa na akinamama na wanaume kujitokeza wakati wa kuvuna na kuuza mazao. Hivyo, kupitia makala hii ya Wanakijiji cha Tandai Kata ya Kinole, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro mkoani Morogoro inatoa mwanga kwa wengine kuona umuhimu wa kushiriki kwa nafasi sawa katika shughuli mbalimbali ili kuhakikisha panakuwepo na maamuzi sawa baina ya mama na kinababa. Pia inatoa mwanga kuwa, ushirikiano baina ya kinamama na kinababa katika shughuli mbalimbali unaimarisha umoja na mshikamano ndani ya familia hivyo kuondoa mivutano hata inapofikia hatua kuwa, kipato kimeshuka au kimepanda. Acceleration of Gender-responsive Sustainable Development Goals localisation
WALENGWA Lengo kuu ni kuwafikishia ujumbe wanajamii ambao huwa na dhana potofu kuwa, jukumu la kinamama ni kulima, lakini baada ya mavuno kinababa ndiyo wenye jukumu la kuuza na kufanya maamuzi ya kipato kinachopatikana. Matokeo yake ni kubadili kabisa hiyo dhana ili pawepo na ushiriki sawa ikiwemo maamuzi ya pamoja. Makala ilichapishwa katika gazeti la Majira Julai 26 na Julai 27, mwaka huu.
NJIA NILIZOTUMIA Mbinu nilizotumia kupata taarifa ni kufika moja kwa moja katika Kijiji cha Tandai Kata ya Kinole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini, niliweza kuwafikia wanakijiji nikawahoji maeneo ya mashambani na masokoni. Niliweza kuhoji zaidi ya watu 15 kati yao wanawake walikuwa tisa na wanaume walikuwa sita. Baada ya kufika katika Kijiji niliweza kujumuika nao moja kwa moja. Dhumuni langu ni kuona namna gani ambavyo kilimo hiki cha viungo kinaweza kusimamiwa vema ili kiweze kuinua wanakijiji hao kiuchumi Acceleration of Gender-responsive Sustainable Development Goals localisation
TIJA/MAFANIKIO Moja ya mafanikio ya awali baada ya kuiandika ile makala na kuichapisha, Kampuni ya Resource Africa Limited na Kampuni ya Organic Group (T) Ltd, zimeonyesha nia ya kwenda kuwajengea uwezo wanakijiji hao baada ya kusikia kutoka kwangu kuwa, wanakijiji hao wanashiriki kwa nafasi sawa yaani kinababa na kinamama katika kilimo cha viungo, hivyo wao muda si mrefu wataenda huko ili kuwapa elimu juu ya namna ya kutumia mbegu bora, kufungasha na ikiwezekana kuwaunganisha na masoko makubwa ili kujipatia mapato zaidi. Acceleration of Gender-responsive Sustainable Development Goals localisation
MREJESHO Mrejesho wa awali katika makala yangu ulikuwa ofisini, wakati wa vikao vya wafanyakazi vya asubuhi, waliguswa na mtiririko wa makala hiyo. Huku wakishauri niendelee kufuatilia zaidi kwa ajili ya kuendelea kujenga jamii katika mtazamo chanya kuhusu ushiriki sawa wa wanawake na wanaume katika shughuli mbalimbali. Pia ninategemea mrejesho zaidi kadri siku zinavyosonga mbele kutokana na ukweli kwamba wasomaji wengi huwa na tabia ya kukaa kwa muda wakitulia ndiyo huanza kusoma vizuri makala, waanze kutoa mrejesho. Acceleration of Gender-responsive Sustainable Development Goals localisation
MWENDELEZO Ninatarajia baada ya hapa kurejea tena Tandai na vijiji vingine ili kuona namna ambavyo, mamlaka mbalimbali zinavyotekeleza wajibu wake katika kuwajengea uwezo wanawake hao ili waongeze nguvu katika kilimo chao ikiwemo mitaji, pembejeo na kuwapa muongozo wa masoko. Pia nitajaribu kufuatilia masoko ya viungo katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwezekana niwaunganishe nayo. Acceleration of Gender-responsive Sustainable Development Goals localisation